6 Julai 2014 - 06:30
Ukraine warudisha mji wa Sloviansk

Jeshi la Ukraine limefanikiwa kuurudisha mikononi mwa serikali mji wa Sloviansk ambao ulikuwa mikononi mwa waasi.

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ameelezea kuwa udhibiti wa mji wa Sloviansk mashariki mwa Ukraine ambao ulikuwa katika mikono ya wapiganaji wanaounga mkono Urusi ni mafanikio makubwa kwa jeshi la serikali.
Wapiganaji hao ambao kwa sasa wamekimbilia katika mji wa Donetsk baada kutekwa kwa Sloviansk na mji wa Kromatosk ambao ulikuwa ngome kuu ya wapiganaji hao, wamesema kuwa:waliuacha mji wa Sloviansk kwa lengola kujiandaa na mapigano mapya.